Kufuatia kesi inayomkabili aliyekuwa Miss Tanzania 2006 Wema Isaack Sepetu kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya bangi, leo hii alitakiwa kusomewa hukumu baada ya jalada la kesi yake kukaa muda mrefu.

Hukumu ya kesi hiyo imesogezwa mbele mpaka Julai 20, 2018 ambayo ni ijumaa ya wiki hii.

Aidha Wema Sepetu amewaomba Watanzania, pamoja na mashabiki wake kwa ujumla kumuombea ili jambo hilo liweze kuisha na kupita salama.

Video: TRA yafunguka makusanyo ya kodi mwaka wa fedha 2017/18
Gonzalo Gerardo kutua Stamford Bridge juma hili

Comments

comments