Ripoti ya Jeshi la Polisi hivi karibuni imesema kuwa kumeibuka wizi wa magari madogo aina ya IST, taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo imesema kuwa wizi umeshamiri na kuwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa kuhusiana na wale wanaojihusisha na vitendo vya wizi.

Dar 24 Media imezungumza na mtaalamu wa mswala ya mifumo ya magari Aziz ambaye amejikita kwenye ufundi wa umeme wa magari.

Amesema kuwa gari aina ya IST ni rahisi kuibiwa kutokana na baadhi ya vifaa vya akiba kufanana, ambapo amesema kuwa mpaka mtu aiba gari anakuwa ameshalijua na anania ya kuiiba, na kutumia funguo wa gari nyingine kuiba.

Bilioni 30 kujenga kituo cha biashara na lojistiki
Vibanda vilivyopo juu ya mitaro viondolewe - Rc Makalla