Siku chache baada ya Wizkid kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Fever’ ambayo inamuonesha Tiwa Savage akiwa kwenye mahaba mazito na mwimbaji huyo, Tiwa amekoreza wino kwa anachoandika mitandaoni.

Tiwa ambaye hakuimba kwenye wimbo huo, ameonekana kwenye video hiyo akimuonesha mapenzi mazito Wizkid kiasi cha kuchochea kuni kwenye moto wa tetesi za wawili hao kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Wakati mashabiki wakiendelea na mjadala wa video hiyo, Tiwa ameandika kwenye Instagram kuwa anayeonekana kwenye video na picha ni ‘Rais wa Pepper Stew Association na mkewe (President and First Lady).

“Introduction: President and the First Lady of the Pepper Stew Association 🌶🌶🌶 #ThisIsAfrica #Beautiful ❤️,” ameandika Tiwa kwenye picha inayomuonesha akiwa na Wizkid.

 

View this post on Instagram

 

Introduction: President and the First Lady of the Pepper Stew Association 🌶🌶🌶 #ThisIsAfrica #Beautiful ❤️

A post shared by Tiwa Savage (@tiwasavage) on


Mbali na picha hiyo, ameweka pia picha ya pozi la mahaba mazito na mwimbaji huyo na kumsifia kwa mafanikio ya video hiyo akivunja rekodi yake mwenyewe na kwamba ndio sababu yuko naye. Ndani ya siku nne, video ya Fever imetazamwa zaidi ya mara milioni 3.

Mkali huyo wa ‘Ojuelegba’ na mwenzake wa ‘Lova Lova’ wamekuwa wakionekana pamoja kwenye matamasha na matukio mengine kama ilivyo kwa wapenzi lakini waliendelea kusisitiza kuwa ni marafiki tu.


Septemba mwaka huu, mume wa zamani wa Tiwa Savage, Teebillz aliandika ujumbe akisaidia kukanusha tetesi za uhusiano kati ya wawili hao, akidai kuwa Wizkid ni mdogo wake na kwamba Tiwa pia anamheshimu na hivyo hawawezi kuwa na uhusiano wa mapenzi.

Baadhi ya mashabiki wamemrudia Teebillz wakimkosoa kwa kujitokeza mapema kukanusha asichokijua, huku wakikazia kuwa lisemwalo lipo na kama halipo laja.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 27, 2018
Mo Dewji afanya tendo jema baada ya kuonekana hadharani

Comments

comments