Kufuatia kesi inayowakabili viongozi wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, kesi hiyo imepangwa kusikilizwa leo mbele ya Mahakama ya kisutu baadaa ya viongozi hao kuswekwa rumande siku mbili zilizopita.

Hadi kufikia saa 5:30 asubuhi ya leo vigogo hao wa Chadema walikuwa bado hawajafikishwa Mahakamani.

Baadhi ya Viongozi wa juu wa Chadema wakiwemo wajumbe wa kamati kuu Chadema ambao waliwahi kuwa Mawaziri wakuu wa Tanzania, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa waliokwenda mahakamani kusikikiliza kesi hiyo wameondoka kabla viongozi hao kufikishwa mahakamni, wakidai wanakwenda kushiriki msiba wa mzee Kimesela anayezikwa makaburi ya Kinondoni, Dar.

Kufuatia matukio hayo wananchi waliohudhuria kesi hiyo wameonekana wakiimba nje ya mahakama wakidai haki, kama video inavyoonekana hapo chini.

Aidha, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake watano, leo wanatarajia kujua hatma ya dhamana juu ya kesi inayowakabili.

Twaweza: 70% yamwamini Rais Magufuli
Aliyekuwa Makamu wa Rais afungwa jela kwa udanganyifu

Comments

comments