Mara baada ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Young Africans, Clement Sanga  kujiuzulu, Kamati ya Utendaji kwa kushirikiana na Bodi ya Wadhamini wamefanya kikao cha dharula na kumteua kiongozi mwingine atakayeshikilia nafasi hiyo iliyoachwa wazi.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Afisa habari Yanga, Dismas Ten amesema Kamati ya Utendaji pamoja na Bodi ya Udhamini imemteua Omary Kaya kuwa Kaimu Katibu Mkuu kwa kipindi hiki cha mpito ili kuweza kurudisha utendaji wa kazi na shughuli za kila siku kwenye klabu.

Aidha amesema zipo nafasi kadhaa ambazo zipo wazi, Kamati ya Utendaji na Bodi ya Udhamini inaendelea kushughulikia taratibu husika za nafasi hizo na muda mfupi ujao itawekwa wazi nani atashika nafasi hizo.

Msikilize hapa Afisa habari Yanga akizungumza na vyombo vya habari leo Julai 24, 2018 jijini Dar es salaam.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 25, 2018
Sasa leseni za madereva kuhakikiwa kielektroniki

Comments

comments