Rapa wa Nigeria, Ycee ameungana na mtayarishaji wa muziki na muimbaji wa Afrika Kusini, DJ Maphorisa kupika na kuipakua audio na video ya remix kali ya wimbo wake ulioiteka Afrika ‘Omo Alhaji’.

Video ya remix hiyo ya Omo Alhaji imeongozwa na La Dupont Productions jijini Johannesburg, na ina kila sababu ya kuwa ngoma inayowaamsha mashabiki wengi katika kumbi za starehe na haina shaka itateka tena mawimbi ya redio na TV barani Afrika.

Ycee anasema, “limekuwa jambo kubwa kufanya remix hii, kama msanii ninafurahi kujaribu muziki tofauti. Ulikuwa uzoefu mkubwa na wa kufurahia kufanya kazi na DJ Maphorisa. Ninaamini mashabiki watafurahia remix hii.”

‘Omo Alhaji’ halisi ilitoka Disemba 2015, na ilimpandisha zaidi Ycee kama mmoja wa wasanii wakali kabisa wa hip hop nchini Nigeria.

Baadae aliachia video ya wimbo huo iliyoongozwa na Director Q iliyofanyika Uingereza. Wimbo huo pamoja na video yake viligeuka wimbo wa taifa kwenye chati za redio za TV za Nigeria, kwenye klabu na hata mtaani huku ukiipa umaarufu sentesi: ‘Who’s your Daddy?

Mtuhumiwa ugaidi akutwa amekufa mahabusu
Tanzia: Dk Masaburi afariki dunia