Young Dee ambaye sasa amelibadili jina lake la Paka Rapa kuwa Paka Rasta, ameeleza jinsi alivyoguswa na kupata funzo kubwa baada ya kukutana studio na mbunge wa Mikumi, Joseph ‘Profesa Jay’ Haule.

Akifunguka kupitia The Playlist ya 100.5 Times Fm, alipokuwa akipiga stori na Lil Ommy, rapa huyo alisema kuwa alishangazwa na tabia ya nguli huyo wa muziki wa kizazi kipya, wakati alipokuwa anamshuhudia akirekodi wimbo wake wa ‘Kibabe’.

Paka Rasta alisema kuwa ilikuwa mara yake ya kwanza kukutana na Profesa baada ya kuwa mbunge, lakini alichokuwa akitarajia kuwa huenda kungekuwa na mabadiliko ya kitabia, kiligeuka funzo kubwa kwake.

VIDEO: Coyo MC ataja maajabu yaliyomkuta kwenye show, awagusa Fid Q, Young Killer

“Unajua tangu Profesa awe mbunge sikuwahi kukutana naye. Sasa baada ya Profesa kuwa mbunge nilitegemea kwamba kuna vitu vingebadilika sana kwa Profesa, si unajua kuwa mbunge…!” Alifunguka.

“Sasa nilivyokaa na Profesa nikaona jinsi alivyokuwa anadeal na producer na wadogo zake, nikajifunza kuwa kwenye maisha siku zote unatakiwa uwe humble. Yaani ujishushe ili uzidi kuwa mkubwa,” aliongeza.

Rapa huyo anaendelea kuusukuma wimbo wake mpya wa ‘Bongo Bahati Mbaya’ ikiwa ni sambamba na muonekano wake mpya unaowezeshwa na Q-Boy Msafi.

 

Askofu Gadi anena ya moyoni kuhusu msiba uliotokea jijini Arusha
Hongera Leodegar Tenga - Rais Wa Heshima TFF