Halimashauri ya Wilaya ya Kinondoni imebaini na kutatua ubadhilifu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 687.9 ambazo Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi, Zantel ilifanya katika mkataba wake miaka 7 iliopita, mkataba uliofanyika mwaka 2009.

Akizungunza na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally  Salum Hapi amesema mkataba huo ulikuwa umefichwa, hivyo baada ya kubaini madudu hayo amefuatilia kwa karibu na kutoa muda wa siku 7 kwa Kampuni hiyo kulipa deni hilo kwa Manispaa ya Kinondoni.

Hapi amesema kuwa baada ya kutoa siku hizo Zantel imefanikiwa kulipa kiasi chote cha fedha na tayari fedha hizo ziko mikononi mwa Halmashauri ya wilaya ya Kinobdoni na Manispaa imeamua kuzipeleka moja kwa moja katika ujenzi wa madarasa ya Wilaya hiyo ambapo kuna upungufu wa Madarasa 79 na kupitia fedha hizo yatapatikana madarasa 40 yaliyokamili.

Aidha, Hapi amesisitiza kuwa ameshaanza kuifuatilia mikataba yote ambayo ilikuwa haieleweki ili haki za Serikali zirudi na wote ambao wamehusika na kuvuruga mikataba hiyo pia waliokuwa katika uongozi wakati huo habari zao tayari zipo katika vyombo vya sheria na haki itatendeka

Azam FC yawatema makocha wake
Yanga kuinyemelea Simba leo? Lwandamina afanya yake