Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli leo Oktoba 31, 2016 ameanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais Uhuru Kenyatta. Rais Magufuli amepokelewa rasmi na kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na baadaye kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.

Mara baada ya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli ameongea na waandishi wa habari katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya, amesema Kenya inaongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania ikilinganishwa na nchi nyingine za Bara la Afrika, hivyo amewakaribisha wafanyabishara wengi zaidi wa Kenya kuwekeza nchini Tanzania

Amesema kuwa biashara kati ya Tanzania na Kenya imeongezeka kutoka shilingi Bilioni 652.9 hadi shilingi za Kitanzania Trilioni 2.044 hivyo amewakaribisha wafanyabishara wengi zaidi wa Kenya kuwekeza nchini Tanzania

Arsenal Yaacha Wanne Safari Ya Bulgaria
Mwana FA akosoa nyimbo za Nigeria kubeba shindano la Miss Tanzania 2016