Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ametembelea chuo cha taifa cha utalii kilichopo jijini Dar es salaam, nakujionea jinsi chuo  hicho kinavyotumia mfumo mbovu wa kufundisha taaluma hiyo inayojihusisha na huduma za utalii hapa nchini.

Waziri Maghembe ametembelea chuo mapema leo Oktoba 19, 2016 ambapo amekagua maeneo mbali mbali chuoni hapo ikiwa ni pamoja na hoteli ya chuo hicho na kukuta baadhi ya sehemu kama za jikoni siyo safi kama inavyotakiwa kwa hoteli.

Wakati akizungumza na wafanyakazi chuoni hapo amesema chuo hicho lazima kiwe na Bodi ya taaluma inayoendana na masomo yanayofundishwa pia kuwepo na wakuu wa masomo ya cheti na diploma na si kukimbilia kutoa degree, kwani lengo ni kutoa  wataalamu walioiva katika taaluma husika na wenye uwezo wa kufanya kazi katika hoteli kubwa. Bofya hapa kutazama video

Serikali: Wanafunzi watakaoandikishwa darasa la kwanza waripoti na mche wa mti
Mkuu wa Mkoa Arusha atoa ujumbe mzito baada ya kuzushiwa ‘ametumbuliwa’