Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia tiketi ya Chama Cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa Bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha 2018/19, inawaumiza wafanyakazi na wakulima nchini.

Ameyasema hayo wakati akifanya uchambuzi wa Bajeti hiyo, mbele ya waandishi wa habari, na wadau wa uchumi na biashara.

Amesema kuwa utekelezaji wa Bajeti hiyo utapungua kwa 23% huku wakulima na wafanyakazi wakiendelea kuumia kama kawaida.

Aidha, amesema ili kuwapa unafuu wananchi amependekeza kuwa Kodi ya mshahara ipunguzwe na michango kwenye mifuko ya jamii ifanyiwe marekebisho ikiwemo kushushwa kwa michango ya pensheni kutoka 20% mpaka 12% ili kuwapa unafuu wafanyakazi na waajiri.

Hata hivyo, Kuhusu kilimo amesema Bajeti yake imepunguzwa kwa 23% licha ya kukabiliwa na changamoto nyingi, huku kikiajiri 66% ya Watanzania wote.

 

 

Video: Basi la King Musukuma laua watu 6, Bajeti zawabana mafisadi kila kona...
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 18, 2018