Aliyekuwa Katibu wa (UVCCM) mkoa wa Kigoma ambaye kwasasa amehamishiwa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Agustino Matefu amesema kuwa atamburuza mahakamani mbunge wa Kigoma mjini kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe kwa madai kuwa sio raia wa Tanzania,

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amedai kuwa ushahidi wote anao.

“Kwasasa nimeamua kwenda mahakamani kumfungulia kesi Zitto Kabwe, sababu sio raia wa Tanzania, nimesafirisha wazee wanne kutoka Kigoma kwa ajili ya kutoa ushahidi,”amesema Matefu

 

Sababu za ‘tumbua-tumbua’ wizara ya madini zaanikwa
Mume wa Amber Rutty aanguka gafla mahakamani