Katika mabadiliko hayo yaliyofanywa na Rais John Magufuli, Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ameachwa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Zitto aliandika kuwa;

“Ndugu yangu Mwigulu Nchemba karibu back bencha ufanye kazi ya wananchi. Tunajua msimamo wako kuhusu barua ya KKKT (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania) umekuponza, ulikuwa na msimamo madhubuti na ulisimamia haki.”Hapo hapo mara tu baada ya ujumbe huo, Polepole aliibuka na kumjibu, Zitto Kabwe ni mzee wa kurukia treni kwa mbele.

“Mzee wa kurukia treni kwa mbele ushaanza, mbona unapenda ubashiri na vitendo vya kilozi. Rais hutenda impendezavyo kwa dhamana aliyopewa na Katiba. Sisi tuliohudumu kwenye Serikali na chama tunajua na kuheshimu, usijitatafutie huruma kwa mtu acha kupotosha hiyo si siasa safi.”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na kumteua Mbunge wa Mwibara, Kangi Rugola kuchukua nafasi hiyo.

Aidha, Rais Magufuli amefanya teuzi nyingine ambapo amemteua Musa Ramadhani Sima kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,

Omary Mgumba kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji,

Mhandisi Isack Kamwelwe kuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,

Na Athumani Kihami kuwa Katibu wa Uchaguzi NEC.

Waziri Mbarawa amehamishiwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji akitokea Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 2, 2018
Video: Watu 20 wamefariki dunia na wengine 45 kujeruhiwa katika ajali ya magari manne Mbeya