Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema zoezi la upandaji miti maarufu kama ‘mti wangu’ litakuwa ni endelevu katika wilaya yake, kampeni hiyo iliyobuniwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ina lengo la kubadilisha muonekano wa jiji kutoka kwenye uchafu na kuwa jiji safi na lenye mpangilio.
Mjema ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ambayo yatapandwa miti katika jijini Dar es salaam Octoba 1 mwaka huu, aidha aliongeza kuwa mabadiliko ya muonekano wa jiji yatakuwa na tija zaidi kwa kutoa fursa kwa wananchi kufanya kazi zao.