Vifaranga 6,400 vya kuku kutoka nchini Kenya vimeteketezwa kwa moto jijini Arusha na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), licha ya mfanyabiashara, Mary Matia kuomba kuvirudisha alikovinunua.

Juhudi za Matia kuwabembeleza maofisa wa TFDA kutoviteketeza vifaranga ili avirerejeshe Kenya japo apate sehemu ya fedha zake zilishindikana na badala yake kugeuka kuwa shuhuda wakati vifaranga hao wakichomwa moto.

“Nimewaomba tuvirejeshe Nairobi niliponunua lakini wamegoma, mimi sikujua kama ni makosa kununua viafaranga nchini Kenya, niliataka tu angalau nirejeshewe japo nusu ya hela niliyonunulia lakini wamevichoma na mimi nimengia hasara kubwa,”amesema Matia

Aidha, amesema kuwa siku hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kupitisha vifaranga hivyo lakini anamiliki mabanda ya kuku katika eneo la Mianzini katika jiji la Arusha.

Hata hivyo, kwa upande wake Ofisa kutoka TFDA, Obeid Nyasebwa amesema kuwa wamechukua hatua hiyo ya kuviteketeza vifaranga hivyo kwakuwa hawajui usalama wake kutokana na kuwepo kwa taarifa za ugonjwa wa mafua ya ndege.

Real Madrid watatoka leo kwa Tottenham?
Meya wa jiji aomba faragha na JPM