Watu wapatao 72 wameuawa na zaidi ya watu 800 wamekamatwa katika ghasia zilizosababishwa na maandamano yanayoendelea Afrika Kusini, kupinga kwenda jela kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma.

Aidha waandamanaji wamegeuza maandamano hayo kuwa ghasia mwishoni mwa wiki, wakichoma moto, kufunga barabara kuu na kuvamia na kupora maduka huku tume ya Umoja wa Afrika kulaani ghasia zinazoendelea Afrika Kusini zilizosababisha vifo 72.

Naye Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, amelaani vikali vurugu hizo ambazo zimesababisha vifo vya raia na matukio mabaya ya uporaji wa mali ya umma na ya kibinafsi, uharibifu wa miundombinu, ikiwemo kusitishwa kwa huduma muhimu katika eneo la Kwazulu-Natal, Gauteng na maeneo mengine ya Afrika Kusini.

Mamia ya wanajeshi yametumwa kusitisha ghasia na uporaji Afrika Kusini kudhibiti machafuko hayo yaliyoibuka siku tano zilizopita.

Mgodi wa Tancoal kupewa siku 14 kuthibiti maji taka
Miss Tanzania avuliwa uwakilishi miss world