Idadi ya miili ya watu waliofariki katika ajali ya kuzama kwa boti mbili zilizokuwa zimebeba wahamiaji, imeongezeka na kufikia 28 huku takribani watu 130 wanadhaniwa kuwa bado wapo kwenye maji katika fukwe za Djibouti.

Taarifa zilizotolewa na shirika la kimataifa linaloshughulikia wahamiaji (IOM),imesema kuwa boti mbili zilizokuwa zimebeba wakimbizi kutoka Godria Pwani ya Afrika Kaskazini Mashariki, siku ya jumanne majira ya asubuhi zilianza safari kuelekea Uarabuni na baada ya dakika 30 zilizama.

Miili ya wakimbizi watano waliofariki waliweza kuipata mapema siku hiyo huku mamlaka za Djibouti zikiwa zimepata miili mingine 23 hadi kufika siku ya leo.

“Miili 23 imepatikana hadi kufika asubuhi ya leo vikosi vya uokoaji vikiwa vinaendelea kuwatafuta” amesema kiongozi wa uokoaji kutoka Djibouti, Lalini Veerassamy.

Tayari watu wawili wameokolewa wakiwa hai na wameshafikishwa (IOM), ambapo wamesema kuwa wanakadiria kwenye safari yao walikuwa watu 130 katika boti waliyopanda lakini hawawezi kukadiria boti nyingine ilikuwa na wahamiaji wangapi.

Veerassamy ameongeza kuwa Djibouti miaka ya hivi karibuni umekuwa kituo au njia kuu wanayotumia wahamiaji wanaoenda kutafuta kazi nchi za Uarabuni ambapo wengi hutokea Somalia na Ethiopia.

Aidha ameongeza kuwa safari za wahamiaji wengi kuelekea Uarabuni hufanywa kwa njia ya miguu, wakikatisha jangwa mashariki mwa Ethiopia, Djibouti na Somalia kaskazini, na wanapofika Yemen na nchi nyingine za Uarabuni hukumbana na mateso, unyanyasaji wa kingono na utumwa wa kazi.

 

 

 

TANZIA: Mgunduzi wa madini ya Tanzanite afariki dunia
Tanzania na Rwanda zapeta vita dhidi ya ufisadi

Comments

comments