Idadi ya vifo vilivyotokana na mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi ya Irani imezidi kuongezeka, ambapo hadi sasa zaidi ya watu 70 wamepoteza maisha.

Serikali ya nchi hiyo bado inaendeleza zoezi la uokoaji na kuhamisha watu waliokatika mabonde kutokana na taarifa kutoka mamlaka ya hali ya hewa nchini humo kuonesha kuwa mvua itaendelea kunyesha.

Wanawake na watoto ambao ndio waathirika wakubwa wamepewa kipaombele katika uokoaji na kuhifadhiwa sehemu salama huku wanaume wakiagizwa kushirikiana na vikosi vya uokoaji.

Mji ambao watu wake wapo katika hatari zaidi ni Susangerd, ulio na wakazi 50,000, pamoja na miji midogo ya karibu yake ambayo tayari watu wanaendelea kuhamishwa.

Mvua kubwa nchini Iran ilianza kunyesha Machi 19 na kusababisha uharibifu wa zaidi ya miji 1,900, maelfu ya barabara, madaraja pamoja na miundombinu mingine.

Iran ni nchi iliyo na utajiri wa mafuta, tayari makampuni yaliyowekeza katika uchimi huo yamejitolea kuhakikisha wanapunguza maji kwenye makazi ya watu kwa kutumia pampu maalumu.

 

 

 

 

Ajabu! Mtoto wa miaka 6 aozwa kwa mvulana wa miaka tisa
Dkt. Chegeni atimiza ahadi zake jimboni Busega