Klabu bingwa barani Afrika Esperance kutoka Tunisia watapambana na Zamalek ya Misri, katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani humo baadae mwezi huu.

Vigogo hao katika soka la Afrika wamepangwa kukutana, baada ya droo ya ya hatua ya robo fainali kupangwa jana mjini Cairo nchini Misri.

Zamalek wataanzia nyumbani Misri kati ya Februari 28 ama 29, na juma moja baadae watakwenda kumalizia mchezo wa mkondo wa pili nchini Tunisia, ambapo mabingwa watetezi (Esperance) watakua wenyeji.

Mbali na mchezo huo, wawili hao watakutana katika mpambano wa kuwania African Super Cup utakaochezwa Februari 14 nchini Qatar, kufuatia Zamalek kuwa bingwa wa kombe la shirikisho huku Esperance wakiwa mabingwa wa ligi ya mabingwa Afrika mwaka 2019.

Michezo mingine ya hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika iliyopangwa na shirikisho la soka CAF.

Mabingwa mara nane wa Afrika klabu ya Al Ahly ya Misri, wamepangwa kukutana na mabingwa wa mwaka 2016 Mamelodi Sundowns kutoka Afrika kusini.

Raja Casablanca ya nchini Morocco, ambao kwa mara ya mwisho walitwaa ubingwa wa Afrika mwaka 1999, watawakabili mabingwa mara tano wa Afrika TP Mazembe kutoka DR Congo.

Klabu nyingine kutoka nchini Morocco Wydad Casablanca, watakutana uso kwa macho na mabingwa wa Afrika mwaka 2006 Etoile du Sahel, kutoka Tunisia.

Ratiba ya nusu fainali pia ilipangwa katika hafla hiyo iliyofanyika Misri na kuhudhuriwa na maafisa/wajumbe wa CAF kutoka nchi mbali mbali za Afrika:

Raja Casablanca/TP Mazembe v Zamalek/Esperance

Wydad Casablanca/Etoile du Sahel v Al Ahly/Mamelodi Sundowns

Wakati huo huu shirikisho la soka barani Afrika (CAF) lilipanga michezo ya hatua ya robo fainali kombe la shirikisho.

Zanaco (Zambia) v Pyramids

Al Nasr (Libya) v Hasania Agadir (Morocco)

Al Masry (Misri) v RS Berkane (Morocco)

Enyimba (Nigeria) v Horoya AC (Guinea)

Hatua ya nusu fainali.

Zanaco (Zambia) v Pyramids (Misri) VS Enyimba (Nigeria) v Horoya AC (Guinea).

Al Nasr (Libya) v Hasania Agadir (Morocco) VS Al Masry (Misri) v RS Berkane (Morocco)

Eric Abidal: Tulisitisha kumsajili Aubameyang
Waziri Mkuu amjibu Mbowe, ''Vyama vya siasa havijazuiwa kufanya shughuli zake''