Maofisa waandamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA) Tawi la Kariakoo Jijini Dar es salaam na mfanyakazi mmoja, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala wakikabiliwa na makosa ya kujipatia shilingi milioni 66 kwa njia ya rushwa.

Maofisa hao ni Liberatus Rugumisa, Keneth Mawere na mfanyakazi mmoja Nasoro Nasoro wote wakazi wa kigamboni Jijni Dar es salaam.

Aidha, Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Lupyana Mwakatobe amesema kuwa washtakiwa hao walitenda hayo kwa madai ya kumpunguzia kodi mfanyabiashara Humphrey Lema kinyume cha sheria.

Mwakatobe amesema kuwa Novemba 18, mwaka huu maeneo ya Ofisi za TRA Kariakoo Wilaya ya Ilala,Rugumisa na Mawere, walijipatia sh.milioni 50 kutoka kwa Lema kwamba wanampunguzia kodi ya ongezeko  la thamani (VAT), pia Novemba 28 mwaka huu walijipatia shilingi. milioni 10.kutoka kwa mfanyabiashara huyo kwa madai ya kumpunguzia VAT.

Hata hivyo Mwakatobe amesema, shtaka la tatu linalo wakabiri ni watuhumiwa hao ni la kijupatia rushwa ya dola 2,774 sawa na shilingi milioni sita za kitanzania kutoka kwa Lema kwa lengo la kumpunguzia VAT, kitu ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yao.

Washtakiwa wamekana mashtaka hayo na kurudishwa rumande kwa kushindwa masharti ya dhamana.

 

Wahukumiwa kwenda jela miaka 73 kwa kosa la kuua tembo
#HapoKale