Kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wanne wa Kampuni ya Mawasiliano ya Six Telecoms imeahirishwa baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi haujakamilika.

Katika kesi hiyo inayomhusisha wakili maarufu nchini, Dkt. Ringo Tenga, mfanyabiashara Peter Noni, Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Hafidhi Shamte, Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Noel Odeny Chacha na Kampuni yenyewe ya Six Telecoms Limited.

Aidha, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo Wakili wa Serikali Leonard Challo ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kesi hiyo upelelezi haujakamilika.

Hata hivyo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 26 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa tena.

Simba SC yamtambulisha rasmi Pierre Lechantre
Kamati ya maadili yatangaza maamuzi dhidi ya wabadhilifu