Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula ameagiza kuundwa tume ya uchunguzi wa eneo la Isamilo jijini Mwanza lenye Viwanja 39 linalolalamikiwa baada ya kununuliwa na viongozi wa Serikali.

Dkt. Mabula ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari wa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2022/23, kilichofanyika jijini Mwanza Julai 13,2022.

Wananchi hao wamelalamima kuwa licha ya wao kujaza fomu za ununuzi wa eneo hilo, bado walipewa viongozi hao na wananchi hawakulipwa fidia.

Juni 2, 2022, Jiji la Mwanza lilitangaza kuuza viwanja katika eneo la Isamilo na kila mwombaji alitakiwa kulipia Tsh. 20,000 ya fomu ambapo baadhi ya Wananchi wamedai kulipia lakini hawakupata majibu.

Dkt. Mabula ameeleza kuwa suala la kuomba viwanja linakuwa wazi kwa mtu yoyote.

“Kilio cha Mwanza tumekisikia ya kwamba wakilalamikia viwanja vya Isamilo kwamba wamepewa vigogo watupu, kama Wizara nimeishamuelekeza Katibu Mkuu aweze kuunda tume ije kufanya uchunguzi, ili kuona ni halali au malalamiko hayo ni ya kweli,” ameeleza Dkt. Mabula.

“Kama waliomba kwa utaratibu ambao wameomba wengine hapatakuwa na kesi kama wamezunguka nyuma ya mlango kama wanavyosema basi litakuwa ni jukumu jingine, naomba nisitoe maelekezo maana niliishatoa maelekezo baada ya kuona kilio hicho kwenye magazeti na luninga,” aliongeza.

Afariki katika shindano la unywaji pombe
UN yalia malipo duni Wafanyakazi sekta ya Afya