Shirikisho la soka nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Azam na Simba.

Viingilio vya mchezo huo  ambao utafanyika kwenye uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam, vitakuwa shilingi elfu kumi (Sh 10,000) kwa Jukwaa Kuu ambalo lina uwezo wa kubeba mashabiki 1,000 tu walioketi, wakati mzunguko (popular) kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu saba tu (Sh 7,000).

Kutokana na changamoto ya uwanja wa Azam Complex kuchukua idadi ndogo ya mashabiki, TFF imewataka wanafamilia ya soka kukata tiketi kuanzia leo Jumatano Septemba 6, ili kujiepusha na usumbufu wa aina yoyote.

Hata hivyo TFF wametoa tahadhari kwa mashabiki ambao hawatokua na tiketi za kuingia uwanjani siku hiyo, kutokwenda Azam Complex kwa lengo la kuepusha msongamano ambao hautokua na lazima.

Vyombo vya usalama vitakuwa makini kudhibniti kila aina ya vurugu uwanjani hapo hasa ikizingatiwa kuwa mchezo huo utafanyika wakati jua limezama. Mchezo utakuwa Septemba 9, 2017 saa 1.00 (19h00).

JPM kupokea ripoti ya kamati ya uchunguzi wa Madini
Rais Karia aunda kamati ya tuzo