Shirikisho la soka nchini, TFF limetangaza viingilio katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (AFCON U20) 2019 yatakayofanyika nchini Niger kati ya wenyeji Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Katika mchezo utakao chezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari za michezo, Ofisa habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo amesema kiingilio itakuwa shilingi 1,000 kwa majukwaa ya mzunguko, wakati majukwaa ya VIP A, B na C mashabiki wataingia kwa Sh. 3,000.

Kikosi cha DRC kimewasili jana usiku jijini Dar es Salaam na kesho jioni kitafanya mazoezi Uwanja wa Taifa kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa jumamosi, Machi 31 kwenye uwanja huo.

Aidha, Ngorongoro Heroes ambayo ipo chini ya kocha Ammy Conrad Ninje itaingia kwenye mchezo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda michezo ya kirafiki dhidi ya Morocco 1-0 na Msumbiji 2-1.

Ikumbukwe kuwa vijana hao wa timu za taifa za Tanzania na Congo wanakutana siku chache baada ya kaka zao “Taifa Stars’’ na ‘The Leopards” kucheza mchezo wa kirafiki ambapo Taifa Stars iliibuka na ushindi wa bao 2-0

Kodi yamsweka rapa jela
Twaweza: 70% yamwamini Rais Magufuli

Comments

comments