YANGA SC imetaja viingilio viwili tu katika mchezo wake wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DRC Jumanne Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam , Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro amesema viingilio hivyo ni Sh. 7000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 30,000 kwa VIP.
Muro amesema tiketi zitaanza kuuzwa Jumatatu jijini Dar es Salaam kuelekea mchezo huo ambao utaanza Saa 10:00 jioni.

Huo utakuwa mchezo wa pili wa Kundi A kwa Yanga, baada ya Jumapili kufungwa 1-0 na wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia Jumapili.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limechanganya marefa watatu kutoka nchi tatu tofauti kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.
Hao ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O’michael wa Eritrea

Rais Barack Obama kununua moja ya vilabu vya kikapu nchini Marekani
Gavan Jeanne: Tumekuja Kujifunza Kwa Wenzetu Tanzania