Keshokutwa Jumamosi, February 10, 2018, Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa kuumana na St Louis ya Ushelisheli kwenye mchezo wa kwanza ligi ya mabingwa barani Afrika, hatua ya awali.

Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na lengo moja tu la kuibuka na ushindi mnono ili kujiweka katika nafasi nzuri na hatimaye kufuzu hatua inayofuata.

Tayari viingilo vya mchezo huo vimewekwa hadharani ambapo VIP A ni Tsh 10,000/- huku VIP B na C ikiwa Tsh 7,000/- wakati mzunguuko ni Tsh 5,000/-

Washelisheli wajifua Tanzania kuivaa Yanga
Evra mambo safi West Ham Utd