Katika kupambana na changamoto za Ajira kwa vijana nchini Shirika la kimataifa la kazi ILO kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la uwezeshaji jamii kiuchumi  NEEC leo limewezesha vijana ishirini kupitia mradi wa ajira yangu ulioanzishwa nchini miezi kadhaa iliyopita.

Wakati wa kuhitimisha shindano la Ajira yangu leo, Katibu Mtendaji NEEC Beng’i Issa amesema tatizo la ukosefu wa  ajira nchini bado ni changamoto kubwa haswa ukiangalia Sensa ya watu na makazi 2012 inaonyesha kuwa nusu ya watanzania ni vijana na wengi wao hawana ajira hivyo kama baraza la uwezeshaji uchumi linajukumu la kujitolea kuwezesha vijana kwa njia mbalimbali.

Aidha ametumia muda huo kuwaasa vijana kumi  ambao wamekabidhiwa  ruzuku siku ya leo kuhakikisha wanakuwa na adabu juu ya matumizi ya fedha pia wasimamie mawazo yao ya kibiashara  na kuwa chachu ya kubadili mawazo ya vijana ambao bado wanafikiri hakuna mafanikio pasipo kuajiriwa.

Bi  Beng’i Issa ameyataka mashirika na taasisi binafsi kuweza kuwasaidia vijana wenye mawazo na ujuzi mbali mbali ili waweze kujiajiri na kuacha kuweka masharti ambayo siyo rafiki kwa vijana ili kutoa dhana ya kuajiriwa na waweze kufanya shuhuli za kimaendeleo kwa kubuni miradi mbali mbali itakayowakwamua kutoka kwenye umasikini .

Akizungumza katika hafla hiyo mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds media group , Ruge Mutahaba wakati akizungumza na vijana hao amewataka vijana wote nchini kusimamia mawazo yao na wasikubali kuyumbishwa na maneno au vikwazo

”fuata kile unachokiamini na simamia unachokitaka” Amesema Ruge Mutahaba

ruge

Nae mkurugenzi wa shirika la ILO ukanda wa Afrika Mashariki Bi. Mary Kawar amesema kuwa shirika hilo halijajikita kutazama  vijana 20 tu kupatiwa ruzuku bali linaangazia Tanzania nzima kuhakikisha kwamba tatizo la ajira linapungua kama siyo kuisha kabisa.

Akizungumza kwa niaba ya vijana walioshinda Gilbert Tarimo muhitimu wa chuo kikuu cha kilimo SUA mwenye mawazo ya kufungua kampuni ya uuzaji wa nyama ya sungura amewataka vijana wenye mawazo ya kujikwamua kiuchumi waamke na kuanza kuyafanyia kazi ”mawazo katika biashara ni mtaji wa kutosha”

Shindano la Ajira yangu lilitangazwa miezi mitatu iliyopita ambapo vijana zaidi ya 831 wenye umri kati ya 18-35 walituma mawazo yao ya biashara katika mchujo wa awali walipatikana vijana 50 na  siku ya leo juni 13 walipatikana vijana ishirini ambao katika kumi bora walipatiwa ruzuku kutokana na mahitaji yao huku kumi waliobakia wakipatiwa milioni 3.2 kila mmoja kwa ajili ya kujiendeleza na ujasiriamali.

 

Salute kwa Wabunge kufyeka mishahara ya Polisi
Video: Waziri Mkuu awataka viongozi wa dini kushirikiana na Serikali kupambana na Rushwa, Ufisadi