Vijana Mkoani Mwanza, wamebuni mradi wa mabegi yanayokusanya nishati ya jua, ili kuwasaidia wanafunzi waishio vijijini kujisomea nyakati za usiku, ikiwa ni harakati za kufanikisha lengo namba nne la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGs la elimu bora, yenye usawa na kutoa fursa kwa wote.

Ubunifu wa mradi huo, uliopewa jina la ‘Soma Bag’ unaenda kutatua shida ya Wanafunzi wengi hasa wanaoishi maeneo ya vijijini, ambao wamekuwa wakikabiliana na changamoto nyakati za usiku inayowalazimu kutumia kibatari ama taa za chemli kupata mwanga wa kujisomea.

Wanafunzi wakiwa wamebeba Begi zenye solar nchini Ivory Coast. Picha ya The Standard.

Muasisi wa mradi huo, Innocent James amesema wazo lilianza wakati wakijaribu kutatua changamoto ya wanafunzi kujifunza wenyewe na kuanza kuwajengea tabia ya kujisomea kwa kuanzisha maktaba tembezi, ambayo ilikuwa ikiwafuata watoto popote walipo.

Kusoma kwa kwa kutumia kibatari ama taa za chemli hutajwa kuwa ni kikwazo katika ufaulu wa wanafunzi kutokana na kuhitaji kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya kununulia mafuta ya taa, ambayo hutumika kuwashia nishati hiyo.

Raila Odinga ataka Wakenya kususia ulipaji kodi
Odinga aanza mapambano kumuondoa madarakani Rais Ruto