Vijana ambao ni sehemu ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 15, Asaad Ali Juma, Maziku Aman, Issa Abdi, Kelvin Deogratias, Athumani Maulid walikua wamekwenda kufanya mazoezi kwenye klabu ya Orlando Pirates, nchini Afrika kusini wamerejea nyumbani.

Vijana hawa waliongozana na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi huko Afrika Kusini walifanya mazoezi ya juma moja kuanzia Septemba Mosi mpaka tarehe 7 Septemba, 2015 chini ya uangalizi wa Augusto Placious ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Orlando Pirates.

Idara ya ufundi ya Orlando Pirates imejiridhishwa na viwango vya wachezaji hao na hatua inayofuata ni mawasiliano kati ya shule wanazosoma hapa Tanzania na klabu ya Orlando Pirates ili kutafutiwa nafasi za masomo kwenye shule za Afrika Kusini.

Jambo hili likikamilika vijana hao watakwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya masomo na kufundishwa mpira.

TFF inamshukuru Dr. Irvin Khoza Rais na mmiliki wa klabu ya Orlando Pirates kwa ushirkiano na kutoa nafasi kwa vijana wa U15 Tanzania kwenda kufanya mazoezi kwenye klabu hiyo kongwe nchini Afrik Kusini na kuendelezea

Kipyenga Cha FDL 2015-16 Kupulizwa Kesho
Mourinho: Inatosha Kufungwa Nyumbani