Taasasi za kiraia zinazounda Umoja wa AZAKI za juu ya masuala ya Bunge kwa kushirikiana na asasi zingine wamekuja na mapendekezo katika kuboresha Sera ya Taifa ya Vijana ya mwaka 2007 ili iendane na wakati pamoja na mabadiliko ya kiteknolojia.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) ambayo ni Asasi kiongozi. Suleiman Makwita wakati akiwasilisha muhtasari wa uchambuzi wa Sera hiyo.

Amesema kuwa lengo la kufanya mapitio juu ya Sera hiyo ni kuangalia namma ambayo wanaweza wakaishauri Serikali maeneo ya kufanyia maboresho katika Sera hiyo ya vijana.

“lengo la kufanya uchambuzi huu ni kuiomba Serikali na wadau wote wa maendeleo ya vijan nchini kuweka mazingira rafiki yatakayochochea maeneleo ya vijana kupitia sekta rasmi na zisizo rasmi ikijuisha masuala mtambuka na kuendana na dhana ya maelengo endelevu ya dunia” amesema Makwita.

Aidha,katika  matokeo ya uchambuzi huo wamebaini baadhi ya changamoto zilizopo katika Sera ya Vijana ya Mwaka 207 na hatimaye wamekuja na baadhi ya mapendekezo kama njia ya kusaidia kuiboresha Sera hiyo.

Hata hivyo, Baadhi ya mapendekezo waliyokuja nayo ni pamoja na kuanishwa kwa umri wa kijana kuwa miaka 13 -35 tofauti na sasa ambapo kijana anatambuli kuwa na umri kati ya 15 hadi 35.

 

Video: Mawaziri kitanzini, Lowassa aionya Kenya na vurugu za uchaguzi
Magazeti ya Tanzania leo Julai 16, 2017