Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imetoa shilingi milioni 70.5 kwa vikundi 21 vya vijana, wanawake na walemavu ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mwaka 2004 yenye adhima ya kuwainua wananchi kiuchumi ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Manispaa hiyo imedhamiria kutekeleza maelekezo ya serikali kwa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani na kuwezesha vikundi hivyo ambapo tangu mwaka wa fedha 2018/2019 uanze mwezi Julai hadi mwezi Novemba Halmashauri tayari imeshakusanya Shilingi bilioni 1.1 ambayo ni nusu ya makusanyo ya malengo waliyojiwekea kwa mwaka huu.

Fedha hizo zilitolewa katika hafla fupi ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo aliyekabidhi hundi kwa vikundi hivyo na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dkt. Khalfan Haule, Meya wa Manispaa ya Sumbawanga, Justin Malisawa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na vikundi husika.

Aidha, Mkuu wa mkoa Rukwa, Joachim Wangabo ameipongeza Manispaa ya Sumbawanga na kwaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri zizlizopo Mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanatekeleza agizo hilo ili kuweza kukuza kipato cha mwananchi wa Mkoa kwa kuwawezesha kiuchumi na hatimae kuongeza ajira pamoja na kukuza uchumi wa viwanda.

“Serikali haitafurahishwa kuona fedha zilizokopwa zinatumika kwa malengo ambayo hayakukusudiwa kama vile anasa, nitoe wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote ndani ya mkoa wetu kupitia hafla hii, kuweka mipango na mikakati ya kuhakikisha wananchi wanawezeshwa kiuchumi.

Hata hivyo, kuanzia mwaka 2013/2014 hadi 2017/2018 fedha zilizopaswa kuchangiwa na Halmashauri hiyo ni asilimia 10 ya mapato ya ndani ni shilingi 684,055,823.

 

Chadema watetea hatua ya mbunge wao kuingia na Ilani ya CCM Bungeni
TRC yafufua reli inayounganisha Tanzania na Uganda

Comments

comments