Wadau wa mazingira wamekutana na wanafunzi wa vyuo vikuu Jijini Dar es Salaam ili kuzungumza nao  kuhusiana na changamoto zinazowakabili vijana hasa katika upande wa uwekezaji pamoja na utambuzi wa fursa zilizo mbele yao.

Akizungumza na Dar24Media Mkurugenzi wa Human Dignity and Environmental Care HUDEFO Sara Pima amesema kuwa wameamua kuwakutanisha wanachuo hao lengo ikiwa ni kuwaelimisha vijana umuhimu wa uwekezaji ili kupunguza changamoto za ajira.

Ameongeza kuwa wamewakutanisha wanachuo hao na wadau mbalimbali sekta binafsi na serikali wakiamini ni njia nyingine ya kumjengea kijana kupata mawazo mkakati na kuyafanyia kazi katika kuleta maendeleo ya Nchi, lakini pia kumjenga kijana kujua njia gani apite na kusimamia malengo aliyonayo yatakayomsaidia kujiajiri hata atakapomaliza chuo.

“Semina za kuwakutanisha wadau mbalimbali kuzungumza nao inasaidia kwa kiasi kikubwa inamjengea kijana kupanua wigo wa mawazo,” Amesema Sara.

Aidha ameainisha mikakati ya HUDEFO ikiwemo pamoja na kuwasaidia vijana katika uelimishaji na kushirikiana nao pamoja kutambua fursa za mazingira hasa katika mabadiliko ya tabia nchi, fursa kwenye afya, kilimo na sekta nyinginezo ili kusaidiana na srikali katika swala la vijana kufikia malengo ya maendeleo endelevu.

Ametoa wito kwa vijana kuacha visingizio, kulalamika na kulaumu bali kuamka na kuwa wabunifu wa vitu tofauti vitakavyosaidia nchi kimaendeleo.

Shabiki wa Simba SC awasili Dar es salaam
Rais Samia afanya mazungumzo na Rais Xi Jinping