Muda wa mwisho uliowekwa kwa vikosi vya kijeshi vya kigeni kuondoka nchini Libya umekamilika jana Januari 23,2021 bila ya kuwepo kwa dalili yoyote kwamba vikosi hivyo vilikuwa vinaondoka.

Mnamo Oktoba 23, 2020 pande hasimu nchini Libya zilifikia makubaliano ya kusitisha mapigano kwenye mazungumzo yaliyofanyika mjini Geneva, Uswisi, yakijumuisha tarehe ya mwisho ndani ya miezi mitatu ya kuondolewa vikosi vya askari wa kigeni na mamluki.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa na kundi moja la kimataifa linalofuatilia hali ya nchini Libya zilisisitiza uungaji wake mkono wa mkataba huo na kutoa wito kwa viongozi nchini humo kuharakisha utekelezaji wa mkataba huo ikiwa ni pamoja na kuondolewa mara moja kwa vikosi hivyo vya kigeni nchini humo.

Libya imekuwa na misukosuko tangu kuondolewa mamlakani kwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Gadafi mnamo mwaka 2011 na taifa hilo limekuwa eneo la vita kwa pande mbili pinzani.

Marekani yailaani Urusi kwa unyanyasaji
Simba SC yamtambulisha kocha wake mpya