Mapigano makali yamezuka tena nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya vikosi vya jeshi la taifa na kundi la waasi linaloendesha hujuma mashariki mwa nchi hiyo la M23.

Vyanzo vya kiraia, maafisa wa jeshi la Congo na kiongozi mmoja wa kundi la M23 vimesema, mashambulizi ya makombora yamepiga ngome za kundi la M23 huku Serikali ikitumai kuikomboa miji ambayo kundi hilo limeikamata hivi karibuni.

Wapiganaji wakilenga shabaha wakati wa mashambulizi huko DRC. Picha ya Reuters.

Maeneo yanayotajwa kuwa na mapambano makali ni ya wilaya ya Rutshuru pamoja na eneo jingine karibu na mbuga ya wanyama ya Virunga iliyopo mkoa wa Kivu Kaskazini.

Hata hivyo, mapambano hayo yalikuwa yamesimama kwa muda wa wiki moja, baada ya kundi la M23 kupata mafanikio kwa kuyakamata maeneo kadhaa, yaliyopo eneo la mashariki mwa DRC.

Matumaini mapya uzinduzi mradi wa Maji Kigamboni
Rais mstaafu aishitaki Kamati ya Bunge