Mshambuliaji aliyewahi kutamba na klabu za Arsenal na Real Madrid, Emmanuel Adebayor, amemshangaa beki wa kati wa Yanga, Vincent Bossou, akidai kiwango alichonacho beki huyo alitakiwa awe anachezea timu kubwa barani Ulaya.

Adebayor, ambaye ni nahodha wa Timu ya Taifa ya Togo, amekoshwa na kiwango cha beki huyo ambacho amekionyesha katika michezo kadhaa timu hiyo yaTaifa ikicheza na timu nyingine.

Bossou alisema Adebayor amemhakikishia kuwa atafanya kila namna ili kumtafutia sehemu ya kwenda kucheza huko Ulaya, ambako ndiko kwenye hadhi yake.

“Yule ni kama kaka yangu, kwani kwenye timu ya Taifa ni nahodha, ameniambia uwezo wangu ni mkubwa na kwamba atatafuta timu ambayo naweza kuchezea barani Ulaya,” alisema.

Akizungumzia hatua hiyo ya Adebayor ya kutaka kumpeleka Ulaya na kuachana na Yanga, alisema yeye anachohitaji ni changamoto mpya na kwamba dili hilo likitiki atawaaga Yanga, kwani wameishi kwa furaha na upendo.

“Kama atafanikiwa kunitafutia timu wala sitakataa kwenda, kwani kila mchezaji katika Bara hili la Afrika anatamani kwenda kucheza Ulaya, nadhani hata Yanga hawawezi kunikatalia, kwani nimeishi nao vizuri na wangependa mafanikio yangu,” alisema.

Bossou alionyesha uwezo mkubwa na kuisaidia timu yake katika kuwania kufuzu michuano ya fainali za Afrika dhidi ya Djibout, akifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 5-0.

Real Madrid Kuweka Vizuizi Kwa Bale, Ronaldo, Pepe Na Modric
Wenger Awakataa Wachezaji Vijana, Asema Walimpotezea Muda