Meneja wa klabu ya AC Milan Vincenzo Montella amekanusha kuwa katika mipango ya kutaka kumsajili kiungo kutoka nchini Hispania na klabu ya Chelsea Cesc Fabregas itakapofika mwezi januari mwaka 2017.

Taarifa zilidai kuwa AC Milan wanajipanga kumsajili Fabregas kama mbadala wa Riccardo Montolivo, ambaye kwa sasa anaendelea kujiuguza majeraha ya goti ambayo yatamchukua muda wa miezi sita ili aweze kurejea tena uwanjani.

Montela amesema ni kweli wanahitaji mchezaji anaecheza nafasi ya kiungo, lakini sio wa aina ya Fabregas ambaye amedai hatoweza kukidhi hitaji la kufikia malengo aliyojiwekea kwa msimu huu.

Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Italia amedai kwamba, Fabregas ni mchezaji mzuri lakini kwa aina ya mfumo wa AC Milan hatoweza kuonyesha cheche zake kutokana na ushindani uliopo katika ligi ya nchini Italia ambayo imekua na utofauti mkubwa na ligi za Hispania na Uingereza.

Image result for Cesc Fabregas not an option to replace Montolivo at AC Milan - MontellaRiccardo Montolivo akiugulia maumivu ya goti wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Hispania.

“Tunahitaji mchezaji lakini atakaeweza kukidhi vigezo tunavyovitaka katika kipindi hiki ambacho tunasaka namna ya kutimiza malengo tuliojiwekea hadi mwishoni mwa msimu” Alisema Montela

Montela anatarajia kumtumia kinda Manuel Locatelli kama mbadala wa Riccardo Montolivo, japo amekua haridhishwi na uwezo wake ambapo mara kadhaa amewahi kunukuliwa na vyombo vya habari vya Italia, akisema mchezaji huyo anakabiliwa na tatizo la umri, na ndio maana huwa hamtumii mara kwa mara.

“Nina matumaini makubwa sana Locatelli. Ndio maana nimejipanga kumchezesha katika kikosi changu japo natambua nimemuwahisha sana, kwani kwa sasa ana umri wa miaka 18, na jambo hilo limekua likimpa wakati mgumu wa kuhimili mikiki mikiki ya ligi ya Sirie A,”

“Lakini tunatakiwa kukumbukwa kwamba bado ni kijana mdogo na anapaswa kupewa muda naamini ipo siku ataweza kudhihirisha kiwango chake na kuisaidia AC Milan. ” Aliongeza  Montella

Liverpool, Man Utd Zatahadharishwa Mapema
Jordan Henderson: Southgate Astahili Kukabidhiwa Kijiti