Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania. Alizaliwa Butiama, mkoani Mara pembezoni mwa Ziwa Nyanza tarehe 13 Aprili, 1922. Alifariki dunia14 Oktoba, 1999. Aliiongoza Tanzania toka mwaka 1961 hadi mwaka 1985.

Yeye ni mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea. Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi hii ndiyo ilimpatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la “Mwalimu.” Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiyari baada ya kutawala kwa muda mrefu.

Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo na aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.

Julius Kambarage Nyerere.

Maisha Ya Mwalimu

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 ( katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika).

Alikuwa mojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya babake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma.

Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.

Mapadre wakaona akili yake wakamsaidia kusoma ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia 1943 – 1945. Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia amejihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).

Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary’s ambapo mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti /Uingereza akasoma M.A. ya historia na uchumi(alikuwa mtanzania wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania).

Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam. Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.

Hayati Mwalimu Nyerere akiwa na Rais wa 54 wa Marekani Hayati John Kennedy.

Mwaka 1954 alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika.

Uwezo wa mwl. Nyerere uliwashitua uongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.

Alijiuzuru ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship council na Fourth committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York.

Mwalimu Nyerere akipiga ngoma, pembeni ni mwanaye Madaraka Nyerere

Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo bwana Richard Turnbull ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru. Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960.

Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9/12/1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru na mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa jamhuri ya Tanganyika.

Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.

Sifa zake

Bado anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu na pia ataendelea kukumbukwa na waafrika kote barani hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.

Ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.

Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama. Alipatwa na kansa ya damu (leukemia) na kufariki Uingereza wakati wa kutibiwa katika mji wa London tarehe 14 Oktoba, 1999. Alizikwa mahali pa kuzaliwa kwake, kijiji cha Butiama.

Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage alizaliwa Aprili 13, 1922 Kijijini Butiama Wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule ikiitwa Tanganyika), akiwa ni mmoja wa watoto 26 wa Chifu wa kabila la Wazanaki, Mzee Nyerere Burito.

Upekee

Katika sehemu ya maisha yake, alipofikisha miaka 20, alibatizwa akawa Mkatoliki na Mapadre walibaini kipaji alichonacho wakamsaidia kusomea ualimu katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda kuanzia 1943 hadi 1945.

Na akiwa Makerere alianzisha Tawi la Umoja wa Wanafunzi Watanganyika na pia akajihusisha na Tawi la Tanganyika African Association (TAA).

Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akawa Mwalimu katika Shule ya Sekondari ya St. Mary´s na mwaka 1949 alipata nafasi ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uingereza akasomea Shahada ya Uzamili ya Historia na Uchumi.

Alihitimu mwaka 1952 na alikuwa Mtanzania wa kwanza kusoma katika Chuo Kikuu cha Uingereza na Mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania.

Ajira

Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika Shule ya Sekondari ya St. Francis (Dar es Salaam) ambayo kwa sasa inajulikana kama Shule ya Sekondari Pugu. Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Tanganyika African Association (TAA).

Chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Makerere. Mwaka 1954 alikibadilisha Chama cha TAA kuwa Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko cha TAA.

Katika kipindi cha mwaka mmoja, Chama cha TANU tayari kilikuwa chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika. Uwezo wa Mwalimu Nyerere uliwashtua viongozi wa kikoloni na kumlazimisha achague kufanya kazi ya siasa au abaki na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.

Mwalimu Nyerere katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda.

Alijiuzulu ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta muungano katika kupigania Uhuru na pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Baraza la Udhamini na Kamati ya Nne ya Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani.

Uwezo wake wa kuunganisha watu ili wawe na umoja na mshikamano kutetea haki zao pamoja na kipaji chake cha kujenga hoja, kutetea na kuzungumza kwa ufasaha ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata Uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha kwa aliyekuwa Gavana wa wakati huo, Bw. Richard Turnbull ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa Uhuru.

Uongozi

Tanganyika ilipata Uhuru wake tarehe 9 Desemba, 1961 na Nyerere alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika huru. Mwaka mmoja baadaye, Nyerere alikuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika.
Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika kuleta Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyounda Tanzania baada ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 ambayo yalimtoa madarakani Sultani wa Zanzibar, Jamshid bin Abdullah.

Mwalimu Nyerere na Mkewe Mama Maria Nyerere.

Februari 5, 1977 Mwalimu Nyerere aliongoza chama cha TANU katika kuungana na chama tawala cha Zanzibar cha Afro – Shiraz Party (ASP) na kuanzisha Chama kipya kilichoitwa Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa Mwenyekiti wake wa kwanza.

Mwalimu Nyerere aliongoza Taifa kwa miaka 23 hadi mwaka 1985 alipostaafu na kumwachia nafasi Rais wa Awamu ya pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi. Yeye alibaki kuwa Mwenyekiti wa CCM hadi mwaka 1990 alipostaafu licha ya kuwa aliendelea kuwa na heshima kubwa katika nyanja za siasa ya Tanzania na duniani hadi kifo chake.

Mwalimu Nyerere alitumia muda mwingi kukaa kijijini kwake Butiama huku akilima shambani kwake. Pamoja na hayo, alianzisha Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation mwaka 1996. Aidha, alikuwa mpatanishi wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi. Pia kati ya mwaka 1987 hadi 1990 alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kusini (South Commission).

Machapisho ya Mwl. Julius K. Nyerere.

  • Freedom and Socialism. Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1965-1967 (1968)
  • Freedom & Development, Uhuru Na Maendeleo (1974)
  • Ujamaa – Essays on Socialism’ (1977)
  • Crusade for Liberation (1979)

Mauti

Tarehe 14 Oktoba 1999, ni siku ambayo Taifa la Tanzania halitaisahau kamwe kwani Mwalimu Nyerere aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 77 katika Hospitali ya St. Thomas iliyoko jijini London, Uingereza baada ya kuugua kansa ya damu. Mwili wa Mwalimu ulipokelewa jijini Dar es Salaam tarehe 18 Oktoba, 1999 na kupelekwa nyumbani kwake Msasani.

Tarehe 20 Oktoba, 1999 mwili wa Baba wa Taifa ulipelekwa Uwanja wa Taifa ili Watanzania kwa ujumla waweze kumuaga mpendwa wao. Tarehe 21 Oktoba, 1999 ilifanyika sala ya mazishi ya Kitaifa katika uwanja huo ambayo iliongozwa na Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi walihudhuria ibada hiyo. Watu waliendelea kumuaga Baba wa Taifa Taifa usiku na mchana hadi tarehe 22 Oktoba, 1999 jioni mwili wake ulipoondolewa na kusafirishwa kwenda Musoma na hatimaye ukasafirishwa kwenda kijijini kwake Butiama kwa ajili ya mazishi.

Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mazishi ya Mwalimu Nyerere yalifanyika tarehe 23 Oktoba, 1999 nyumbani kwake huko Mwitongo katika kijiji cha Butiama, wilayani Musoma Vijijini, mkoani Mara.

Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo wa kuona mbali, hata alipopingwa baadaye waliompinga walikiri ukweli wa maono yake. Ni dhahiri kwamba Mwalimu Nyerere anakumbukwa kwa Mambo mengi ya msingi aliyoyapa kipaumbele wakati wa uongozi wake.

jambo mojawapo alilowahi kulisema wakati wa uhai wake julai 29, 1985 ni kwamba “kazi iliyokuwa muhimu kuliko zote kwangu Mimi , ilikuwa ni kujenga Taifa lenye umoja kwa msingi wa heshima na usawa wa Binadamu.” Mwenyezi Mungu Mrehemu.

Djigui Diarra: 2023/24 tutakiwasha zaidi
Zlatan Ibrahimovic: Hata familia yangu imeshtuka