Leo Juni 11, 2018 Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela amesema tayari wamechagua viongozi 900 kwa ajili ya kuanza kufanya uhakiki wa mali za viongozi hao ili kuthibitisha thamani na uhalisia wa mali hizo na kutambua namna walivyozipata.

Amesema kuwa zoezi hlo linatarajiwa kufanyika ndani ya mwezi mmoja kuanzia Juni 18 hadi Julai 18 mwaka huu.

Aidha uhakiki huo unatarajiwa kufanyika kwa baadhi ya viongozi na si viongozi wote Nsekela amesema ni kutokana na Serikali kutokuwa na fedha za kutosha za kuhakiki viongozi wengi kwa wakati mmoja.

“Sasa tumefikia mahali ambapo tuende kuhakiki kwa baadhi ya viongozi nasema kwa baadhi ya viongozi kwasababu kuna sababu nyingi, sababu kubwa tunasema ni rasilimali fedha tunasema kwamba kama fedha hatuna za kutosha hatuwezi kuwahakiki viongozi wengi kwa hivi sasa tumefanya uchambuzi wa viongozi 900 ambao sasa tunakwenda kuwahakiki” Amesema Nsekela.

Lengo kubwa la mchakato huo ni kusimamia vyema suala zima la maadili kwa viongozi hasa katika matumizi ya fedha kwani kumekuwa na lawama nyingi juu ya viongozi kujilimbikizia mali wenyewe bila kuleta maendeleo kwa wananchi wanaowatumikia.

“Kama mnavyojua sisi tunazungumzia suala zima la maadili kwamba kiongozi awe na maadili na mimi kama kiongozi na mmoja wapo wa viongozi nikitoa tamko langu na nikitaka kuhakiki tunataka tujue zile mali nilizo nazo na uwezo wangu kuna uwiano gani hapo, hizo mali nimepata kihalali au sijapata kihalali” Amesema Nsekela

Aidha Disemba 27, 2017 Nsekela aliwahimiza Viongozi wa Umma kukamilisha taratibu za ujazaji wa fomu za tamko la rasilimali na madeni kabla ya Disemba 31 mwaka huo.

Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Tunisia
Kesi ya Mbowe na wenzake yagonga mwamba, wataka rufaa

Comments

comments