Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya mataifa ya Asia na Pasifiki APEC, wameiongezea shinikizo Urusi kuachana na uvamizi inaoufanya Ukraine.

Jumuiya hiyo, iliyo na wanachama 21 imetoa taarifa ya pamoja baada ya siku moja na nusu ya mkutano wao wa kilele uliofanyika Bangkok ambapo baadhi ya wanachama wamevikosoa vita vya Urusi na Ukraine na kuyumba kwa uchumi wa dunia uliochangiwa na mgogoro huo.

Wanajeshi katika uwanja wa vita nchini Ukraine. Picha ya BBC

Hata hivyo, Wanachama wengi waliokosoa vita hivyo vinavyoendelea Ukraine wamesisitiza kuwa vimesababisha mgogoro mkubwa wakibinaadamu, kuudhoofisha uchumi wa dunia, kusababisha mfumuko wa bei, mgogoro wa nishati na ukosefu wa usalama wa chakula.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 20, 2022 
Watoto walia na Serikali ndoa za utotoni