Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu 12, wakiwemo viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Arusha.

Viongozi hao walikamatwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakituhumiwa kuhusika kuchoma moto mashine za kuvuta maji kutoka kwenye chanzo cha Kangdet wilayani Karatu kwa madai kwamba wanatekeleza agizo la Serikali, hatua ambayo imeelezwa kuwa haikufuata utaratibu

Kamanda wa Polisi, Charles MKumbo alizungumza na waaandishi wa habari na kuwataja waliokamatwa kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Karatu, Moshi Darabe ambaye ni Diwani wa kata ya Barai anayedaiwa kuhamasisha wananchi kuchoma moto mashine hizo zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 6

Wengine waliokamatwa ni pamoja na Diwani wa Kata ya Mang’ola, Lazaro Emmanuel, viongozi wa vijiji wa kata hiyo pamoja na baadhi ya wananchi.

Kamanda Mkumbo alisema kuwa msako wa kuwakamata watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo bado unaendelea na uchunguzi utakapokamilika watafikikshwa mahakamni kwa hatua za kisheria.

 

#HapoKale
Video: Darassa afunguka kuhusu Hip Hop, asema heshima haitengenezwi na mtu mmoja