Kufuatia tukio la nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa, Alphonce Muyinga kuteketezwa na moto, viongozi na baadhi ya wanachama wa Chadema wanashikiliwa na polisi kuhusika na tukio hilo.

Ambapo Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa amelaani vikali kitendo cha jeshi la polisi kuwakamata viongozi na wanachama wa Chadema kwa kudai kuhusika na matukio hayo.

Aidha amesema Polisi walipaswa kufanya uchunguzi wa kiintelijinsia ili kujua chanzo cha nyumba hiyo kuwaka moto na nyingine kubomolewa kuliko kufanya uamuzi ambao umepelekea kuwaweka hatiani wasiohusika na uhalifu huo.

“Polisi Iringa acheni mara moja kamata kamata ya Vijana Iringa Mjini kwa tuhuma za kuchomwa nyumba Moto na kubomolewa nyumba. CHADEMA haina visasi vya damu katika ‘struggle’ ya Demokrasia Nchini. Kuhusisha uharibifu wa aina hii na siasa ni kukosa weledi na maarifa katika uchunguzi” alisema Msigwa

Aidha Mchungaji Msigwa amesema kuwa kuhusu nyumba kuungua moto huwa kuna vyanzo vingi vinavyosababisha, polisi walipaswa kwanza kutulia na kuvipa nafasi vyombo husika kuweza kujua chanzo cha moto huo.

 

Pierre Lechantre awasili, kuanza kazi haraka iwezekanavyo
Korea kaskazini na kusini kuishangaza dunia