Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamewasili jijini Brussels nchini Ubelgiji, kuanza mchakato wa kuwateua wakuu wapya watakaopewa nyadhifa za kusimamia taasisi mbalimbali za umoja huo.

Hilo limejiri mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa bunge la Ulaya, ambao ulivitikisa vyama vikuu, ambapo kazi kubwa iliyobaki itakuwa kumteua atakayekuwa rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya.

Rais wa halmashauri hiyo huwa na mamlaka makubwa na hudumu kwa miaka mitano, ambapo kwasasa nafasi hiyo inashikiliwa na Jean-Claude Junker.

Aidha, tayari kuna mabishano makali yamezuka kuhusu nani anapaswa kushikilia wadhifa huo, huku wafuasi wa vyama vya Kihafidhina vinavyounga mkono Umoja wa Ulaya EPP wanadai mgombea wao, Manfred Weber ndiye anayestahili kukabidhiwa wadhifa wa mwenyekiti wa halmashauri hiyo.

Kwa upande wake Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amepinga wazo la kwamba mwenye kuongoza orodha ya wagombea ndiye anayestahili kukabidhiwa wadhifa huo.

Naye Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema kuwa muungano anaoongoza, unaunga mkono wazo kuwa kiongozi wa halmashauri hiyo anapaswa kuwa mwanasiasa aliyewania kiti hicho.

Waziri amsweka ndani mkandarasi
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 29, 2019

Comments

comments