Shirikisho la Utalii nchini Kenya KTF limepinga kauli ya waziri wa utalii nchini humo kwamba Kenya imekuwa ikipoteza watalii, huku wengi wao wakikimbilia Tanzania.

Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mohammed Hersi amesema kuwa Tanzania ni taifa ambalo linakua kwa kasi katika sekta ya kitalii lakini hakuna usindani wowote kati ya mataifa hayo mawili.

Ameyasema hayo mara baada ya waziri wa utalii nchini Kenya, Najib Balala kusema kuwa Kenya imekuwa ikipoteza watalii wake, ambao wamekuwa wakielekea nchi jirani ya Tanzania kutokana na hoteli zake kuchakaa.

“Sababu ambayo Tanzania ilifanya vyema katika sekta ya utalii zaidi ya Kenya ni kwamba hoteli zao ni mpya na za kisasa huku zetu zikiwa zimechakaa na zina umri wa miaka 40,” amesema Balala

Hata hivyo, Kwa mujibu wa waziri huyo, amesema kuwa Utalii uliipatia Tanzania $2.3 bilioni (Sh5 trilioni) mwaka uliopita kutoka $2 bilioni (Sh4.4 trilioni) 2016. Mapato hayo yalikuwa $1.9 bilioni 2015 (Sh4.18 trilioni).

Maelfu waandamana kupinga uamuzi wa Israel dhidi ya Waafrika
Mourinho adai anasubiri muda ufike achukue pointi tatu kwa Chelsea