Uongozi wa klabu ya Arsenal upo mbioni kumsainisha mkataba mpya meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger, ambaye amedumu  zaidi ya mameneja wengine katika ligi ya nchini England kwa sasa.

Taarifa zilizochapishwa na gazeti la The Times, zimeeleza kwamba uongozi wa The Gunners umeshatayarisha mkataba mpya na wakati wowote watakamilisha mpango wa kumsainisha mzee huyo, ambaye anapigwa vita na baadhi ya mashabiki klabuni hapo.

Sababu kubwa ya Wenger kufikiriwa kupewa mkataba mpya, ni mipango madhubuti ambayo amekua akiihakikishia bodi ya klabu hiyo, kwa kaumini kuna nafasi kwa Arsenal ya kutwaa uibingwa chini ya utawala wake.

Hata hivyo imeelezwa kwamba, muwekezaji mkuu wa klabu ya Arsenal, Stan Kroenke amekuwa akivutiwa na utendaji wa kazi wa babu huyo mwenye umri wa miaka 66, ambao umejikita sana katika suala la kuingizia pesa na si kwenye mafanikio ya kutwaa mataji.

 Mmoja wa mashabiki wa Arsenal akionyesha bango lenye ujumbe mzito kuhusu Arsene Wenger 

Hatua hiyo ya kusainishwa mkataba mpya, inatarajiwa kupokelewa tofauti na baadhi ya mashabiki wa klabu ya Arsenal, ambao wamekua mstari wa mbele kwa kutaka kuona Wenger akiondoka na meneja mwingine anatafutwa, ili kutoa mwanya wa kufunguliwa ukarasa mpya wa kusaka mafanikio ya kutwaa mataji.

Kwa mara ya mwisho Arsenal walifanikiwa kutwaa taji la ligi ya nchini England, msimu wa 2014-15 na iliwachukua muda wa miaka tisa kurejesha furaha kwa kutwaa ubingwa wa kombe la FA mara mbili kabla ya msimu huu kurejea kwenye mfumo wa kumaliza bila taji.

Chelsea Wajipanga Kwa Vita Ya Kumuwania Alvaro Morata
Didier Deschamps Ataja Jeshi La Wenyeji - Euro 2016

Comments

comments