Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich amekutana na Bodi ya klabu hiyo kujadili hatma ya meneja wa klabu hiyo, Jose Mourinho.

Hii ni baada ya klabu hiyo kuambulia matokeo mabovu kwa  msimu huu, ambayo yaliendelea kudhihiri mwanzoni mwa juma hili kwa The Blues kukubali kibano cha mabao  2-1 dhidi ya Leicester City.

Kubamizwa huko, ilikua ni mara ya 9 kwa msimu huu kati ya michezo 16 walizocheza mpaka sasa, hali inayohatarisha usalama wa Chelsea kubaki ligi kuu kwa msimu wa 2016-17.

Haijabainika iwapo Mourinho mwenye umri wa miaka 52, bado atakuwa kwenye majukumu yake ya umeneja  wakati wa mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo The Blues watawakabili Sunderland kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Mmiliki wa klabu hiyo ya magharibi wa jijini London, Roman Abramovich alitangaza kuwa na matumaini makubwa na Mourinho mwezi Oktoba, lakini hali imeendelea kuwa tete kwa kuambulia matokeo mabovu.

Abramovich na viongozi wengine wa  Chelsea wamekuwa wakimuunga mkono meneja huyo lakini kuna kizungumkuti cha ni hadi lini watasubiri klabu hiyo iimarike.

Mwanzilishi wa Chadema Amsifu Magufuli, Amshauri
Aliyekuwa Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni Asimamishwa Kazi