Sakata la vurugu ya ‘vutankuvute’ kuhusu kiti cha Uenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) limetajwa kuwa zito na kupelekea kutanda hewa nzito kati ya viongozi wa chama hicho.

Agosti 21, Profesa Ibrahim Lipumba alizua vurugu ndani ya Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho baada ya wapambe wake kutaka zoezi la uchaguzi kuahirishwa na badala yake kumjadili na hatimaye kupitisha barua ya mwanasiasa huyo kutaka kurejeshewa uenyekiti.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya ukumbi ambao mkutano huo ulifanyika na kushindwa kufikia muafaka, viongozi wa ngazi za juu wa CUF waliokuwa meza kuu akiwemo Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad waligoma kumpa mkono wa salam Profesa Lipumba aliyeingia ndani ya ukumbi huo bila mwaliko.

Mashuhuda waliliambia gazeti la Habari Leo kuwa baada ya Profesa Lipumba kuingia ndani, alipita meza kuu kwa nia ya kuwasalimia viongozi hao lakini alikataliwa hata kupewa mkono na hatimaye kuelekezwa kiti cha kukaa.

Katika mkutano huo uliofanyika Agosti 21, ni wajumbe 14 tu kati ya 832 waliopiga kura kutaka Profesa Lipumba arejee kwenye nafasi ya Uenyekiti.

Jana, wanachama 300 wa chama hicho wametangaza kwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kupinga uamuzi unaochukuliwa na viongozi wa chama hicho ambao wamedai unavunja katiba ya chama na kuminya demokrasia.

Lowassa: Chadema ni nani hadi tukapambane na Polisi..?
Kiongozi Wa Boko Haram Ajeruhiwa Vibaya Katika Shambulio Lililofanywa Na Jeshi La Nigeria