Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewaomba viongozi wa dini kukemea baadhi ya maneno yanayotamkwa na wanasiasa badala ya kukaa kimya akiwa.

Ametoa ombi hilo leo Agosti 22, 2020 wakati anaongea na viongozi wa dini visiwani Zanzibar,amesema katika kipindi chote cha uchaguzi viongozi wa dini ni moja ya wadau wa amani nchini.

“Niwaombe sana kwasababu mnasikia baadhi ya maneno yanayotamkwa na baadhi ya wanasiasa lakini mmekaa kimya hamsemi, mmekaa kimya hamkosoi, mmekaa kimya mekuwa woga niwaombe sana ni muda sasa kuona kuna jambo linaenda ndivyo sivyo tulikemee”, – alisema IGP Sirro.

Aidha IGP Sirro amesema kuwa baadhi ya viongozi wa dini hawako kwa ajili ya kusaidia watanzania badala yake wapo kwasababu ya tama waliyonayo ya kutaka madaraka .

Hata hivyo amewaonya viongozi wote wa dini wanaojihusisha na uhalifu kuwa atawachukilia hatua bila kujali nafasi yao katika jamii kwani ukikiuka sheria lazima uadhibiwe kwa mujibu wa sharia.

“Padri ukishajiingiza kwenye uhalifu mimi ntakushughulikia kama uhalifu mwingine, Padri ukishakuwa mbakaji ntakugonga kama mbakaji mwingine, Shehe/Padri ukijiingiza kwenye ugaidi ntakushughulikia kama gaidi hiyo kwasababua heshima ina ukubwa zaidi kuliko mtu binafsi” amesema IGP Sirro.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 23, 2020
Kongamano la kitaifa kuwakutanisha viongozi mbalimbali