Viongozi wa dini na wanasiasa wamejadili na kukubaliana kwenda kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli wakiwa na pendekezo la kukamilishwa kwa mchakato wa kupatikana katiba mpya itakayoongoza nchi bila uminywaji wa demokrasia.

Ambapo viongozi hao wamejadili mada hiyo pindi walipofanya kongamano la viongozi wa siasa na dini lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), na kufanyika jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa (TCD), James Mbatia amesema lengo la kongamano hilo ilikuwa kujadili hali ya nchi kutokana na hofu iliyomo miongoni mwa wananchi, huku kukiwa na malalamiko ya ukandamizwaji wa demokrasia kutoka kwa vyama vya siasa, na kupendekeza kuwa ipo haja ya kujenga taasisi imara za usawa na haki.

Viongozi hao wamelalama juu ya uminywaji wa demokrasia hasa kwa vyama vya upinzani hali ambayo imetandaza hofu kwa wananchi.

Aidha baadhi ya viongozi wamepinga vikali tabia ya jeshi la polisi kutumia nguvu na mabavu kwa wananchi wake na kuwatia uoga.

Vile vile wameomba na kupendekeza uhuru wa katoa maoni uimarishe na kuwataka wadau wa siasa kujiepusha na chuki.

Hata hivyo, mwakilishi wa CCM, Wilson Mukama amesema katiba mpya si kipaumbele cha Serikali kwa sasa.

Tanzia: Mtoto wa Cannavaro afariki dunia
NEC yatao sababu idadi ndogo ya wapiga kura kinondoni na Siha