Jeshi la Polisi nchini Kenya limeendelea kuwasaka na kuwatia nguvuni viongozi wa ngome ya upinzani ya NASA ambapo wikendi iliyopita wamemshikilia mbunge, George Aladwa.

Mbunge huyo aliyekamatwa alikuwa miongoni mwa viongozi wa NASA waliohudhuria tukio la kuapishwa kwa Raila Odinga kuwa ‘Rais wa Watu’ mwishoni mwa mwezi uliopita.

“George Aladwa amekamatwa nyumbani kwake na hivi sasa anashikiliwa katika Makao Makuu ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai,” amesema mwanasheria wake, Nelson Havi.

Imeelezwa kuwa mwanasiasa huyo anahojiwa kuhusu hatua yake na kauli zake kuhusu tukio hilo la kuapishwa kwa Raila.

Huyu ni mwanasiasa wa tatu mwandamizi wa NASA aliyekamatwa na Jeshi hilo. Siku moja kabla, jeshi hilo lilimkamata Miguna Miguna aliyejitangaza kuwa ‘jenerali’ wa vuguvugu la NRM.

Viongozi wa NASA wazidi kunaswa na Polisi
Mgombea udiwani aliyepotea apatikana akiwa hajitambui