Siku chache baada ya mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa kupinga matokeo rasmi yaliyotolewa na NEC yakimtangaza Dkt. John Magufuli kuwa mshindi na Rais Mteule anayesubiriwa kuapishwa, viongozi wa Ukawa wameelekea Ughaibuni kutafuta msaada wa kisheria.

Taarifa kutoka kwa chanzo cha kuaminika zimeeleza kuwa, viongozi hao wameelekea Uholanzi kutafuta msaada ya kisheria ili kufahamu hatma yao kwani wanaamini mgombea wao alishinda nafasi ya urais kwa asilimia 62, takwimu zilizotofautiana na matokeo yaliyotangazwa na NEC yakionesha alipata asilimia 39.97.

“Viongozi wetu wapo Uholanzi kwenye mazungumzo nyeti juu ya kilichotokea, soon watatupa mrejesho. Letz stay calm.!”

UHOLANZI

Taarifa hizo ziliambatana na picha inayomuonesha mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa na mwanasheria wa Chama hicho wakiongea na ‘wazungu’ katika eneo lilitajwa na chanzo hicho kuwa ni Uholanzi.

Hata hivyo, katiba ya nchi hairuhusu matokeo ya urais yaliyotangazwa na NEC kuhojiwa mahakamani.

Wakati Tume ya Uchaguzi ikimtangaza Dkt. John Magufuli wa CCM kuwa mshindi wa nafasi ya urais kwa asilimia 58.46, Mgombea urais wa Chadema Edward Lowassa alidai kuwa takwimu walizonazo kutoka vituoni zinaonesha kuwa yeye ndiye mshindi na alipata asilimia 62 ya kura zote.

Rais Mteule Awatetemesha Walioivuta Shati CCM Wakiwa Ndani
Bomu Lilitegwa Kituo Cha Polisi Lazua Taharuki Zanzibar